Na Stephen Jackson, Kongwa
Wanafunzi wametakiwa kujitambua na kujitunza kiafya kwa kuepuka vishawishi mbalimbali kama sehemu ya Mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ili waweze kutimiza Malengo yao.
Rai hiyo imetolewa siku ya Alhamisi ya Tarehe 26 Oktoba, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, wakati akihutubia katika tamasha la Mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi lililofanyika Shule ya Sekondari Kibaigwa, katika Mamlaka ya mji mdogo wa Kibaigwa.
Katika hotuba yake aliwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kukataa ushauri usiofaa kutoka Kwa baadhi ya wazazi na walezi wenye mwamko duni wa Elimu, ambao wamekuwa wakiwashawishi wanafunzi kuandika majawabu ya uwongo katika mitihani yao ya Taifa Ili wasiendelee na masomo kwa lengo la kuwapeleka kufanya kazi za ndani katika Miji mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliuoandaliwa na waratuibu wa Tamasha hilo, jumla ya Wananchi 41,817 wWilayani Kongwa walipima Maambukizi ya VVU Kwa hiari, na kati yao 1,037 sawa na 2.4% walikutwa na Maambukizi huku 70% ya idadi hiyo wakiwa ni wanawake.
Kwa upande wa huduma za matibabu kwa wanaoishi na VVU, Jumla ya watu 7001 wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU yaani (ARV) ambapo wanawake ni 5013 na wanaume ni 1988.
Taarifa inasema, jitihada madhubuti za kupambana na kasi ya Maambukizi ya VVU hasa utoaji wa elimu zimekuwa zikifanyika Kwa kushirikiana na Wadau kutoka mashirika mbalimbali yakiwemo EGPAF, AMREF, TAYOA, NACOPHA, AFNET.
Tamasha Hilo la Mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi liliandaliwa na Wizara ya Afya, Kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na lilihusisha wanafunzi wa Shule kumi na mbili (12) za Wilayani Kongwa ambapo wasanii mbalimbali akiwemo Stamina, Joh Makini na wengineo walitoa jumbe mbalimbali kupitia burudani zao.
Shule zilizoshiriki ni pamoja na Shule ya Sekondari Kibaigwa, Shule ya Wasichana Kibaigwa, Dr. Nkullo, St. Pio, Christopher, Benjamin, Ndurugumi, Mlali, Pandambili, Zoissa, Songambele, na Hogoro
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.