• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
    • Miradi iliyokamilika
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • Michezo
    • Michezo
    • Sanaa

Wahofia kuchimba mabwawa kwa Mikono

Imewekwa: January 18th, 2023

Na Mwandishi Wetu, Kongwa DC

Wananchi wa Kijiji cha Tubugwe Kibaoni Kata ya Chamkoroma Wilayani Kongwa, wamehofia kuchimba kwa mikono mabwawa ya Kufugia samaki katika mradi wa shamba darasa la ukuzaji wa Viumbe maji.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 119 umepangwa kutekelezwa kiwilaya na Wizara ya Mifugo na uvuvi katika Kijiji cha Tubugwe Kibaoni kama Kituo maalumu cha kujifunzia stadi za ukuzaji wa Viumbe maji.

Wakijadili katika mkutano wa hadhara Januari 17, 2023, Wakazi wa Kijiji hicho waliazimia kutumika kwa zana za kisasa kutekeleza mradi huo kwani lengo lao ni kupata mradi wenye tija na si kunufaika na fedha za utekelezaji mradi.

Akitolea ufafanuzi kuhusu mradi huo, Afisa Mifugo Wilaya ya Kongwa Bwana Msafiri Mkunda, alitaja faida za mradi huo kuwa ni pamoja na kuwapatia lishe bora na kuongeza kipato kwa wananchi kwani mradi utafungua fursa za kibiashara kutokana na wananchi wa Maeneo mbalimbali kuingia Kijijini hapo kupata mafunzo.

Bwana Mkunda ameitaka jamii kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo Ili uweze kukamilika kwa wakati.

Maamuzi hayo ya Wananchi yamefikiwa  katika mkutano wa hadhara uliofanyika Januari 17, katika Ofisi ya Kijiji hicho.

Awali Mhandisi wa Mradi huo Bi. Anitha Kalumuna alieleza ukubwa na kina cha mabwawa ili kujenga uelewa wa wananchi ambapo aliwataka wananchi kutaja mbinu watakayotumia Ili kuzingatia viwango vya Kitaalamu.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Afisa Manunuzi Bwana Samwel Mwamalange, ameitaka kamati itakayoteuliwa kusimamia mradi,  kuhakikisha inafuata Sheria na  taratibu za utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Majadiliano hayo ya kina baina ya Wananchi kuhusu utekelezaji wa mradi yamefikia hitimisho kwamba Kamati ya usimamizi itashughulikia upatikanaji wa Mitambo ya kuchimba mabwawa hayo na wananchi watashiriki kwenye shughuli nyingine kama itakavyoelekezwa.

Uamuzi huo wa wananchi ulikuja baada ya Divisheni ya mifugo kuwapa Uhuru wa kujadili kwenye mkutano wa hadhara jinsi ya kutekeleza mradi huo hususani kwenye uchimbaji wa mabwawa.

Katika mradi huo uliotengewa kiasi cha shilingi milioni 119, jumla ya mabwawa manne yaliyofuatana na yenye vipimo sawa yanatarajiwa kuchimbwa, sambamba na miundombinu mingine iliyoainishwa kwenye mchanganuo wa mradi.

Mkuu wa Divisheni ya Mifugo na Uvuvi Bwana Msafiri Mkunda akitoa ufafanuzi katika mkutano wa hadhara, Januari 17, 2023.

Mhandisi wa Mradi Bi. Anitha Kalumuna akifafanua vipimo vya Kitaalamu vya mabwawa ya Kufugia samaki.

Afisa Manunuzi Bwana Samwel Mwamalange akielezea mambo ya kuzingatia wakati wa utekelezaji mradi

Mmoja wa wasimamizi wa mradi kutoka Kijiji Cha Tubugwe Kibaoni akichangia mada.


Baadhi ya Wananchi wa Kijiji Cha Tubugwe Kibaoni wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara kuhusu uchimbaji wa mabwawa.

Matangazo

  • Kuitwa kwenye Usaili Ajira za muda -TASAF December 02, 2022
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2022 December 01, 2022
  • Kuitwa kazini Ajira za Muda - TASAF December 06, 2022
  • Fomu ya Maelekezo ya kujiunga na shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa. May 18, 2022
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • Viongozi wa kisasa watakiwa kushirikiana na wataalamu

    March 12, 2023
  • Watendaji wote waahidiwa kupewa pikipiki

    February 17, 2023
  • Kongwa kumalizia tatizo la Upimaji Ardhi.

    February 14, 2023
  • Mkurugenzi Kongwa aonya wazazi wanaokatisha tamaa wanafunzi.

    February 13, 2023
  • Tazama Yote

Video

''KONGWA MMEUPIGA MWINGI''
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)
  • Bunge la Tanzania

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 737 798 222

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.