• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
    • Miradi iliyokamilika
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • Michezo
    • Michezo
    • Sanaa

TAKUKURU YAAINISHA WAJIBU WA VIONGOZI WA DINI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI

Imewekwa: October 1st, 2024


Na Bernadetha Mwakilabi, Kongwa


Moja ya wajibu wa viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya rushwa kwanza kabisa wao wenyewe wasijihusishe na vitendo vya rushwa katika kipindi cha Uchaguzi na mahali pengine popote kwani wao kama binadamu wanaweza kukutana na vitendo hivyo na wakashiriki kwa kujua au kutokujua. Hayo yameainishwa katika semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU walipokutana na viongozi wa dini katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mapema wiki hii.

Akiongea na viongozi wa dini, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Kongwa Bwana Cosmas Shauri amesema Rushwa ni dhambi kwa mujibu wa maandiko matakatifu hivyo viongozi wa dini wana wajibu wa kushughulikia rushwa kwa waumini wao kama wanavyoshughulikia dhambi nyingine, ameongeza pia kwamba viongozi wa dini wana kundi kubwa linalotegemea huduma ya kiroho hivyo ni vyema wakatumia nafasi hiyo kuwafundisha na kuwasisitiza madhara ya kuwachagua viongozi wala rushwa.

Aidha Bw. Shauri amewaasa viongozi hao wa dini wasipokee zawadi toka kwa wagombea ili wawaruhusu kutumia nyumba za ibada kufanya kampeni.

Bw Shauri ameelezea kuwa michakato ya Uchaguzi na uteuzi wa wagombea katika vyama vya siasa imekuwa hatarini kwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na udanganyifu, ambapo wagombea wamekuwa wakiwapa wanachama fedha ili waweze kuwachagua na baadhi wamekuwa wakiwanunulia, chakula, pombe na hata kuwasafirisha kwenda kupiga kura.

Bw Shauri ameendelea kwa kuelezea kuwa Rushwa imetajwa katika  maandiko matakatifu katika Qur'aani tukufu sura ya 2 aya ya 188 ambayo inasema "wala msiliane mali zenu kwa ubatili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua". Pia katika upokezi utokanao na Swahaba Ibnu Umar amesema "mtoa rushwa na mpokea rushwa Makazi yao ni motoni"

Pia katika Biblia Takatifu Injili ya Luka 3:14 Wakati Yohana Mbatizaji akiwaasa watu watubu,  "askari nao wakamwuliza wakisemea sisi nasi tufanye nini? Akawaambia msidhulumu mtu wala msishtaki kwa uwongo tena mtosheke na mshahara wenu". Pia Injili ya Mathayo 28:12-13 "wakakusanyika pamoja na wazee wakafanya shauri wakawapa askari fedha nyingi wakisema semeni ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku wakamwiba tulipokuwa tumelala".

Bw. Shauri, Pia amefafanua madhara ya rushwa katika Uchaguzi kuwa ni kuondoa uhuru wa mpiga kura, pale wagombea wenye vipaji na uwezo wa kuwasilisha, kushindwa kushiriki kugombea katika Uchaguzi kwa kukosa uwezo wa kifedha, hii hupelekea rushwa katika Uchaguzi kuzuia wananchi kuwapigia kura viongozi wanaowataka.

Ameongeza kuwa rushwa huharibu dhana nzima ya uwakilishi kwa kuwa wanaochaguliwa hawana ridhaa kamili ya mpiga kura lakini pia viongozi waliochaguliwa kwa njia ya rushwa hawawezi kusimamia mapambano dhidi ya rushwa wakiwa madarakani na usimamizi wa shughuli za maendeleo hukwama kutokana na vitendo vya ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Bw. Shauri amehitimisha kwa kusema kuwa madhara ya rushwa katika jamii huikumba jamii yote ambayo viongozi hao wapo, hivyo nao ni waathirika wa madhara hayo lakini wakiungana wote kwa umoja wao wataweza kupunguza rushwa kwa kiwango kikubwa katika nchi yetu.

Kwa upande wake Afisa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU Wilaya ya Kongwa Bwana Severine Kisuda amesema Uchaguzi ni mchakato ambao watu wa eneo la Uchaguzi wanatumia kutafakari mustakabali wa maendeleo yao katika eneo na lengo lake hasa ni kupata viongozi waadilifu waaminifu watakaojali maslahi ya jamii kwa kuhakikisha wanawaongoza wananchi kuweka mipango ya kuendeleza eneo lao na kulisimamia.


Afisa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU Bw. Severine Kisuda akitoa elimu kwa viongozi wa dini.


Kisuda amesema baadhi ya wanasiasa hupenda kutumia rushwa ili kuingia madarakani kwa kuwarubuni wapiga Kura ili wawachague hivyo wananchi watambue umuhimu wa kushiriki Uchaguzi kwa ustawi wa maendeleo yao na Taifa hivyo waache kuchagua viongozi wanaogawa zawadi fedha nguo chakula n.k.

Amewasihi viongozi wa dini kutoa elimu kwa wananchi kushiriki Uchaguzi bila kujihusisha na vitendo vya rushwa kuepuka vurugu machafuko vita mauaji na ghasia, na kuwaeleza kuwa wanaweza kutoa taarifa kwa kufika ofisi za TAKUKUKURU  au kupiga simu ya Bure  namba 113.

Akiongea kwa niaba ya viongozi wengine wa Dini Shekh Iddi Binde wa msikiti Masjid Qubaa amesema wamepokea mafundisho hayo na kuahidi kushirikisha waumini katika kila ibada wanazofanya kuanzia Sasa ili watambue vitendo na viashiria vya rushwa hususani katika kipindi hiki cha Uchaguzi ili wawatambue na wachague viongozi watakaowaongoza vizuri na kuwaletea maendeleo.

Kikao hiki ni muendelezo wa vikao ambavyo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa imeendelea kufanya na makundi mbalimbali yenye ushawishi katika jamii ili kuelimisha na kutoa elimu ya rushwa kipindi ambacho nchi yetu inaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa. TAKUKURU imeendelea kusambaza ujumbe kwa kutumia kauli mbiu yake isemayo, Kila mmoja wetu akisema , “nazuia rushwa katika uchaguzi ili nipate viongozi waadilifu na watakaotekeleza kwa ufanisi mipango ya maendeleo.” Tutakuwa tumemshinda adui rushwa.


Matangazo

  • Majina ya mipaka ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. October 16, 2024
  • TANGAZO LA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 16, 2024
  • Tangazo la nafasi za ajira za mkataba October 07, 2024
  • Tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu- Oktoba 1 2024 October 02, 2024
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • MGOGORO WA MPAKA CHIGWINGWILI - HOGORO KUTAFUTIWA UFUMBUZI.

    May 08, 2025
  • VIKUNDI VYASISITIZWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI NA VIONGOZI PAMOJA NA WATAALAM

    May 05, 2025
  • VIKUNDI 21 VYAKABIDHIWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI

    April 28, 2025
  • DC MAYEKA AKABIDHI MISAADA

    April 27, 2025
  • Tazama Yote

Video

zoezi la uandikishwaji daftari la Mpiga Kura kuanza 11-20 Oktoba, 2024
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Time huru ya Uchaguzi
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 713399349

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.