Na. Mbonea E. Masha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Dr. Omary Nkullo amepewa zawadi ya pongezi na Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa kwa kazi nzuri ambayo ameendelea kufanya toka alipoanza kazi katika nafasi hiyo.
Akimkabidhi zawadi hiyo, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa amesema kuwa kazi kubwa anayofanya Mheshimiwa Omary Nkullo inaonekana na ni wajibu kutoa pongezi ili kuendelea kuhimiza na kuhakikisha kuwa kazi inafanyika na wananchi wanapata maendeleo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi, mheshimiwa Dr. Omary Nkullo ametoa shukrani zake za dhati kwa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa na kuongeza kuwa zawadi aliyopata ni chachu ya yeye kuendelea kufanya kazi kubwa zaidi kwa maslahi mapana ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na wananchi wake kwa ujumla.
Zoezi la utoaji zawadi limefanyika katika Ukumbi wa chama cha mapinduzi wilayani Kongwa katika mkutano wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi kujadili taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.