Sunday 8th, December 2024
@Kata ya Ugogoni
Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Kongwa kuendelea tarehe 22 Januari 2018.
Mtumishi wa Ofisi ya NIDA Wilaya ya Kongwa Ndugu Agness Kaliza ameeleza kwamba zoezi hili kwa wiki ijayo kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 28 kwa Kata ya Ugogoni na baadaye wiki inayofuata kuhamia katika Kata ya Sejeli (tarehe 29 Januari 2018 hadi 4 Februari, 2018).
Aidha, ameeleza kwamba zoezi hili lilianza mwaka jana na hadi sasa asilimia kubwa ya wakazi wa tarafa ya Kongwa wameshaandikishwa na kupatiwa vitambulisho vyao.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.