Biashara ni sehemu ya maisha ya wanajamii wa Kongwa kwa sasa.
Kuna muamko mkubwa watu wa rika mbalimbali kujishughulisha za biashara za aina mbalimbali kama usafirishaji wa mazao, na uchakataji wa mazao katika hatua mbalimbali kabla ya kupelekwa sokoni.
Kutokana na muamko huu, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kupitia mradi wa uboreshaji wa mazingira ya biashara (LIC) imejenga Kituo cha Biashara (OSBC) ili kurahisisha utoaji wa huduma ya kupata leseni ya biashara ndani ya muda mfupi na sehemu moja. Jengo hilo linahusisha ofisi zote zinazohusika katika mchakato wa kupatikana kwa leseni - Ardhi, Mazingira, Biashara, Mapato, TRA na Benki.
Aidha, hapo utapata huduma ya kusajili kampuni kwa njia ya kielektroni katika tovuti ya BRELA na simu ya mkononi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.