• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • OSBC

DC Kongwa Awataka Viongozi Kuacha Kuchochea Migogoro

Imewekwa: August 12th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndg. Dkt. Suleiman Serera awahasa viongozi wa kata ya Ngomai kucha mara moja mchezo wa kuchochea migogoro. Ameyasema haya katika ziara yake kwa Tarafa ya Mlali, iliyoanza katika Kata ya Ngomai, leo tarehe 11 Agosti, 2020.

Katika mkutano wake na wananchi wa Kata hiyo ya Ngomai, imebainika kwamba baadhi ya viongozi ndiyo wamekuwa sehemu ya migogoro iliyoibuka kati ya wakulima na wafugaji kwani baadhi yao wamekuwa wakiwakaribisha wafugaji kutoka Wilaya ya Kiteto kuingiza mifugo yao kinyume na sheria ambayo imekuwa ikiharibu mashamba ya wakulima na kuiua migogoro mara kwa mara.

“Kiongozi yeyote atakeyebainika kuwa sehemu ya mgogoro atachukuliwa hatua kali za kisheria; Viongozi msiwe vigeugeu katika kusimamia kesi; Wahusika wasimamie majukumu yao kikamilifu, waache uchochezi wa migogoro” alisema Ndg. Dkt Suleiman Serera.

Aidha, katika mkutano huo amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wananchi wa Kata ya Ngomai.

Baadhi ya kero kubwa ya wananchi wa Ngomai ni eneo lao kuwa na umeme mdogo na kushindwa kuendesha shughuli za viwanda; mgogoro wa mpaka kati ya Kijiji cha Chilanjilizi Kata ya Ngomai na Kijiji cha Silale kilichopo Kata ya Makawa; Kijiji cha Ngomai kukosa maji ya kutosha; Kitongoji cha Kawawa kutosambaziwa umeme toka mradi wa REA kuanza mwaka 2016 na Kijiji cha Saigoni kukosa Mtendaji wa Kijiji.

Kero hizo zote zilijibiwa, ambapo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa ametoa, maelekezo na maagizo kwa wahusika toka sekta za ardhi, umeme na maji kuhakikisha wanashughulikia kero hizo ndani ya kifupi.

Aidha, Ndg. Dkt Serera ameiagiza TAKUKURU kumfuatilia na kumkamata Mhandisi mshauri wa mradi wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Manyata ambaye ametoroka baada ya kuharibu mradi katika Kitongoji cha Kawawa.  

Ziara hiyo kwa tarehe 11 Agosti, 2020 iliishia Kata ya Njoge lakini kutokana na msiba hakuweza kufanya mkutano na wananchi wa kata hiyo kutokana na msiba ambapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoge alifiwa na baba mkwe. Aidha, Ndg. Dkt. Serera alifika msibani kutoa pole na kujitambulisha kwa wananchi walikuwepo msibani hapo, alitoa rambirambi ya shilingi 100,000/-kwa wafiwa.

Ziara hii yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kujitambulisha rasmi itaendelea kwa Kata za Chiwe na Kibaigwa tarehe 12 Agosti, 2020; Kata za Lenjulu na Pandambili tarehe 13 Agosti, 2020.  Ziara hii inaongozwa na kauli mbiu ya “Kongwa Tumefanikisha Mengi, Pamoja Tuyaboreshe na Kunufaika zaidi”.


Matangazo

  • Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2021 December 17, 2020
  • Tangazo la Nafasi ya Kazi November 18, 2020
  • Mabadiliko ya Mawasiliano ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya October 23, 2020
  • Kuitwa Kwenye Usahili November 13, 2020
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • Spika Ndugai akabidhiwa Hati ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa

    October 30, 2020
  • Kituo cha Afya Ugogoni Chaanza Kutoa Huduma za Upasuaji

    August 12, 2020
  • DC Kongwa Awataka Viongozi Kuacha Kuchochea Migogoro

    August 12, 2020
  • Rais Magufuli Aongea na Wananchi wa Kongwa

    July 18, 2019
  • Tazama Yote

Video

MHE. JOB Y NDUGAI AIBUKA KIDEDEA KWA MARA NYINGINE TENA | BILA KUPINGWA | CCM | KONGWA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)
  • Bunge la Tanzania

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 737 798 222

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2020 Kongwa District Council . All rights reserved.